IQNA

Fainali za Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani  ya Iran:

Kundi la Kwanza la wanawake laonyesha uwezo wao wa kusoma  Qur’ani Tukufu

11:51 - January 29, 2025
Habari ID: 3480114
IQNA – Kundi la kwanza la washiriki katika kitengo cha wanawake lilipanda jukwaani Jumamosi asubuhi kuonyesha ujuzi wao wa kusoma Qur’ani Tukufu  katika hatua ya fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani  ya 41 ya Iran.

Baada ya Asma Falaki, qari wa heshima, kusoma aya kutoka katika Qur’ani  Tukufu, washiriki walianza kupanda jukwaani kulingana na ratiba yao.

Washiriki katika kitengo cha wanawake siku ya kwanza ya fainali walikuwa:

Zaynab Abdul Rahman kutoka Ghana (mhifadhi  Qur’ani  yote),

Masoumeh Mohammadi kutoka Afghanistan (Tarteel),

Ifnan Rashad Ali Yaqub kutoka Yemen (amehifadhi),

Jamliaya Abdulqadir kutoka Ufilipino (Tarteel),

Hana Ali Mirafi kutoka Nigeria (amehifadhi),

Hura Haydar Hamzi kutoka Lebanon (Tarteel), na

Karima Haj Brahim kutoka Thailand (Tarteel).

Kipindi cha asubuhi kilihitimishwa kwa usomaji wa Quran na qari mwingine wa heshima, Marziyeh Mirzaeipour.

Mashindano katika kitengo cha wanaume yanafanyika katika vipindi vya alasiri.

Wasomaji na wahifadhi wa Qur’ani Tukufu  kutoka nchi 144 walishiriki katika hatua za awali za mashindano haya, na kutoka kwao, wawakilishi kutoka nchi 27 wamefanikiwa kufika katika hatua ya fainali kwenye vipengele vya wanaume na wanawake.

Fainali hizi, zinazofanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad, kaskazini-mashariki mwa Iran, zitafikia tamati katika hafla ya kufunga ambapo washindi wa juu watatangazwa na kutunukiwa tuzo.

Mashindano ya Kimataifa ya Qu’rani  ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaliwa kila mwaka na Shirika la Awqaf na Masuala ya Hisani la nchi hiyo.

Lengo lake ni kukuza utamaduni na maadili ya Qur’ani Tukufu  miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi wa Qu’rani.

 

 

3491632

 

captcha